AHADI ZA BWANA KWA WANADAMU.

Mungu wetu anatuwazia mema na anatuahidi mambo mazuri na makuu sana hapa duniani pia mbinguni.
Biblia inatuonesha Mungu alivyo waahidi watu wa misri kuwa wasiogope kwani yeye yupo upande wao atawapigania ISAYA 43:1-5.
Hata hivyo Mungu anatuahidi kuwa atakuwa nasi katika mafuriko ya taabu,shida,masumbuko,na yote yanayofanana na hayo.
Mungu anatuahidi zaidi maisha mazuri huko mbinguni baada ya kufa.

Ili Mungu aweze kututimizia ahadi zake yatupasa kuyafanya haya.
1.kufuata mafundisho na maonyo tunayopewa na wazazi,walezi na watumishi wote wa Mungu.
2.Nguvu zetu zitumike kuombea na kusaidia wahitaji hasa wajane,wazee yatima na wasiojiweza (kiroho na kimwili)
3.Kudumu katika sala na kuwasaidia walio maskini wa roho.
4.Kumkiri Bwana kwa kinywa chako na kumtangaza kristo katika hadhara (WAFILIPI 2:11)
5.Kutokuwa na ubaguzi yaani kuonesha upendo kwa kila mtu (1kor 13:13)
6.Kuepuka na kukaa mbali na dhambi yaani kuwa na usafi kamili wa mwili na roho kama YUSUFU pia BIKRA MARIA mama wa MUUMBA(KRISTO).

Hivyo basi wapendwa wana wa Mungu tunahaswa zaidi na kristo kuenenda kwa roho wala si kwa mwili kamwe hatutazitimiza tamaa za miili na roho zetu zenye dhamiri mbaya (Wagalatia 5:13-20)

Mwisho naamini wote kwa pamoja tukijinyenyekeza na kutii mafundisho na kukubali kung'ang'ania imani yetu kuwa kama ya nyumba ya YAKOBO ,tutabarikiwa kwa wakati na ahadi za bwana tutatimiziwa kwa wakati.

MUNGU AWABARIKI NA AMANI YA KRISTO IWE PAMOJA NANYI NYOTE .AMINA
Share on Google Plus

About CLETUSKAMANYI BLOG

4 comments:

  1. Amina kaka Cretus kwa ujumbe mzuri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante nawe pia nashukuru kwa kuendelea kufanya vyema kazi ya Mungu.

      Delete
    2. Asante nawe pia nashukuru kwa kuendelea kufanya vyema kazi ya Mungu.

      Delete
  2. Amina kaka Cretus kwa ujumbe mzuri.

    ReplyDelete