Matendo ya huruma na toba ya kweli!

Nimeona vyema niwakumbushe ujumbe huu wa mwaka jana


Matendo ya huruma na toba ya kweli!

Mwilisheni matendo ya huruma: kiroho na kimwili katika maisha yenu ya kila siku!

14/03/2016 07:57
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika ujumbe wake wa Kwaresima kwa Mwaka 2016 linatafakari kwa kina na mapana kuhusu huruma ya Mungu; ufunuo wa huruma ya Mungu kwa mwanadamu; Kanisa na huruma ya Mungu. Leo katika Makala ya Hazina Yetu, Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inaendelea kukushirikisha kuhusu matendo ya huruma: kiroho na kimwili; umuhimu wa toba ya kweli, Bikira Maria Mwenyehuruma na hatimaye, hitimisho la Ujumbe wa Kwaresima kutoka kwa Maaskofu Katoliki Tanzania.

Matendo ya huruma
“Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma”. Kristo Bwana wetu anatufundisha na kututaka kuwatendea wanadamu wote kwa mapendo na huruma. “Kama Baba yenu”. Hiki ndicho kipimo. Mungu ndiye kipimo cha upendo na huruma ambao wanadamu wanaalikwa kuudhihirisha katika maisha yako. Tunapowatendea wenzetu matendo ya huruma tunamtendea Kristo mwenyewe anayetueleza uwepo wake kwao. “Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitenda mimi (Rej. Mt 25:40). Mapendo na huruma yakikristo si ya vionjo bali ya hitaji. Mungu anatupenda sisi si kwa sababu tunavutia, bali tunavutia kwa sababu anatupenda na kutuhurumia daima (Rej. Kum 6:5, Law 19:8). Hivi tunapopendana kuhurumia jirani zetu, tunawafanya wavutie na kupendeza na tunaufanya uumbaji uvikwe kwa sura yake ya uhalisia wa awali inayovutia.
Mapendo kwa jirani yana msingi wake katika kumpenda Mungu. Ndiyo maana Yesu anasisitiza kuwa, kumpenda Mungu kuende sambamba na kumpenda jirani (Rej. Mt 22:39). Jirani ni mtu yeyote, mhitaji. Mfano wa Msamaria mwema unasisitiza fundisho hilo (Rej. Lk 10:25-37). Na sheria yote na manabii inategemea amri hiyo ya Mapendo (Rej. Mt 22:40). Kumpenda Mungu ina maana pia kupenda vyote vinavyopendwa na Mungu. “Kwahiyo, huruma kwa masikini na wagonjwa, vilevile matendo ya huruma ya ujima, yenye lengo la kupunguza kila aina ya dhiki za wanadamu, yanaheshimiwa na Kanisa kwa namna ya pekee… Utendaji wa huruma leo waweza kuwaelekea watu wote kabisa na mahitaji yao, na lazima uwe wa namna hiyo. Kila mahali wapo watu wenye kukosa chakula, na kinywaji, mavazi, makao, madawa, kazi na elimu, na vifaa vinavyohitajika ili kuweza kuishi maisha yaliyo kweli ya kiutu. Wapo wanaohangaika katika dhiki au kwa sababu ya kukosa afya, wanaoteseka mbali na makwao au walio kifungoni, na hapo mapendo ya Kikristo lazima yawatafute na kuwapata, kuwaliwaza kwa uangalizi mkarimu na kuwainua kwa kuwapatia msaada.”
Tunapenda basi kuwakumbusha tena mafundisho ya Kanisa letu juu ya matendo ya huruma ya mwili na ya roho. Mapokeo ya Kanisa letu yanatufundisha juu ya matendo saba ya mwili, ambayo Kanisa limechota toka Maandiko Matakatifu (Rej. Mt 25:36; Tobit 1:17).
(i) Kuwalisha wenye njaa
(ii) Kuwanywesha wenye kiu
(iii) Kuwavika wasio na nguo
(iv) Kuwakaribisha wasio na makazi
(v) Kuwatembelea wagonjwa
(vi) Kuwatembelea wafungwa
(vii) Kuwazika wafu.
Tukifanya hivyo, huruma ya Mungu itakuwa wazi kwetu na kwao. “Katika parokia zetu, jumuiya zetu, vyama vyetu vya Kitume na vikundi, katika maana kwamba popote alipo Mkristo; kila mmoja apate chemchemi ya huruma.” Kusoma, kutafakari na kusikiliza Neno la Mungu ni msaada mkubwa katika kutembea kwenye njia ya huruma. Pamoja na matendo hayo ya huruma ya mwili mapokeo ya Kanisa yanatufundisha pia kutenda matendo ya huruma ya roho yanayotupeleka kuwajibika katika:
(i) Kuwashauri wenye mashaka
(ii) Kuwafundisha wasiojua
(iii) Kuwafariji wenye huzuni
(iv) Kuonya wakosefu
(v) Kusamehe makosa
(vi) Kuvumilia wasumbufu
(vii) Kuombea wazima na wafu
Jamii yetu inajumuisha watu wenye uwezo mkubwa na wenye uwezo mdogo. Wengine ni wazee, watoto, wagonjwa na walemavu, n.k. Tunawahimiza walio na uwezo kuwasaidia wasio na uwezo. Haya ni makundi ya watu wanaotuzunguka kila siku na huu ni uhalisia wa maisha. Tujifunze kumwona Yesu katika wahitaji hawa na tutambue kuwa
Share on Google Plus

About CLETUSKAMANYI BLOG

0 comments:

Post a Comment