Maana ndefu ya Ishara ya msalaba

Maana ndefu ya Ishara ya msalaba
_Ishara ya msalaba ina maana ndefu sana!_

1. _Kukiri ukombozi wetu ulipatikana kwa Yesu Kristo kupitia msalaba_

2. _Kukiri utatu Mtakatifu yani Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu!_

3. _Tunaposhikanisha vidole vitatu wakati wa kufanya ishara ya msalaba, tunajiunganisha na Mungu katika nafsi tatu au tunapotumia vidole vyote vitano, tunakili madonda matano ya Yesu kristo!_

4. _Tunatumia mkono wa kulia kufanya ishara ya msalaba (unaomanisha mamlaka)_

5. _Tunapoanza kufanya ishara ya msalaba tunaanzia kwenye paji la uso kisha kifuani au kitovuni (ikimaanisha Mungu Baba alimtuma mwanaye kutoka juu mbinguni na kuja duniani)_

6. _Tunaelekea bega la mkono wa kushoto kisha kulia (hii inamaanisha Yule aliyetumwa kutoka mbinguni kuja duniani, alitutoa katika uovu (kushoto) na kutuleta katika wokovu (kulia)_

7. _Baada ya kukiri vyote hivyo tunafunga mikono ambayo dole gumba hupishana kwa kutengeneza namna ya msalaba! Kama ishara kuu iliyotumika katika kumnyanyua yule tunaemwabudu yaani (Kristo Yesu)_

_Na mwisho tunasema Amina tukimaanisha iwe hivyo (yaani tudumu katika ukombozi huo
Share on Google Plus

About CLETUSKAMANYI BLOG

0 comments:

Post a Comment