Uzalishaji wa vitunguu wenye tija, udhibiti wa Wadudu na Magonjwa ya Vitunguu

Uzalishaji wa vitunguu wenye tija, udhibiti wa Wadudu na Magonjwa ya Vitunguu

Zao la vitunguu hulimwa duniani kote kwa ajili ya kutumika kama kiungo cha chakula. Kila familia angalau hutumia kitunguu mara moja klia siku katika chakula chao. Vitunguu hutumika kama dawa katika baadhi ya jamii na wataalamu wanasema hupunguza shinikizo la juu la damu na kupunguza matatizo mengine ya moyo.

Ili uweze kuzalisha mazao ya jamii ya kabichi unahitaji vitu vifuatavyo:

i) Ardhi yenye rutuba.

ii) Mbegu bora ya vitunguu; k.m Red Creole kutoka ktk chanzo cha kuaminika

iii)  Uwezekano wa kupata maji.

iv)  Dawa za kudhibiti magugu, wadudu na magonjwa.

Uchaguzi wa mbegu bora
Mbegu bora ichaguliwe kwa kuzingatia sifa zifuatazo:

1)     Iwe na ustahimilivu dhidi ya magonjwa na wadudu.

2)     Yenye kutoa mavuno mengi.

3)      Inayokomaa mapema ilu kuwahi soko.

4)     Inayoendana na hali ya hewa ya eneo shamba lilipo.


Uchaguzi wa eneo kwa ajili ya kitalu na shamba:
Udongo – vitunguu ni zao la kina kifupi, udongo uwe laini na usio na mawe wala mabonge ili kuruhusu ukuaji wa kitunguu. pH ya 6-7 na usiotuamisha maji.

 Hali ya hewa: joto la sentigredi 15 – 25


Kupanda moja kwa moja shambani
Ingawa zipo baadhi ya faida za kupanda mbegu za vitunguu moja moja kwa moja shambani (direct seeding) kama kuepuka usumbufu wa kutunza kitalu, njia hii sio maarufu sana miongoni mwa wakulima ukilinganisha na ile ya kutumia kitalu. 

Miche ya vitunguu itakua tayari kwa kupandikizwa kati ya wiki 6 hadi 8 baada ya kupanda kitalu. Wakati wa kupandikiza, itawanye mizizi sawasawa kadri ilivyojipanga katika shina kabla ya kufukia na kushindilia kiasi.
Muhimu; wiki mbili kabla ya kuhamisha miche kutoka kwenye kitalu kwenda kuipandikiza shambani, unatakiwa kuipa miche mazingira halisi ya shambani kwamfano kupunguza kiwango cha maji na kuiondolea kivuli. Hii husaidia kupunguza uwezekano wa miche kufa pindi inapo amishiwa kwenye mazingira mapya ya shamba.

Wadudu waharibifu wa vitunguu
Jina la mdudu

Thiripi (Thrips): Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na shina. Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na kusababisha majani kuwa na doti nyeupe. Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake jambo ambalo huathiri mavuno pia.
Thrips huudhibitiwa kwa kunyunyuzia dawa iitwayo Protrin 60 EC.
 
Kimamba: Wadudu hawa hufyonza maji kwenye vitunguu, na kusambaza ugonjwa wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu. Wadudu hawa ni hatari zaidi kwa kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi kwenye mbegu.
Wadudu hawa huthibitiwa kwa kunynyuzia dawa Metakan super 350 SE



Sota (Cutworms): Sota au viwavi wa nondo wanasababisha uharibifu mkubwa. Viwavi wanakata mashina ya miche michanga sehemu ya chini ya shina juu ya ardhi. Sota wanapendelea kula wakati wa usiku na mchana kujificha kwenye ardhi karibu sana na sehemu waliokata shina. Uharibifu huu unapunguza sana idadi ya mimea shambani na kuleta upungufu wa mazao.
Wadudu hawa wanadhibitiwa kwa kupulizia dawa kama; PROTRIN 60 EC, Agromectin 1.8 EC ambayo hutumika ndani ya wiki 0-7 na Metakan super 350 EC nayo hutumika ndani ya wiki 8-20.

Utitiri wekundu (Red spider mites)
Hawa ni wadudu wadogo sana, ambao wanajificha upande wa chini wa majani. Wanafyonza maji maji kwenye majani na kusababisha majani kuwa na rangi nyeupe. Wadudu hawa wanatengeneza utando mweupe kuzunguka majani na mashina. Mmea unashindwa kutengeneza chakula na baadaye inakufa.
Njia ya kudhibiti:
kupulizia dawa za wadudu AGROMECTINE 1.8 EC.

 Vipekecha majani (leaf miner)
Hawa ni aina ya inzi wadogo, ambao viwavi wake wanashambulia majani, kwa kupekecha na kutengeneza mitandao wa mitaro kwenye majani. Viwavi wanashambulia majani na kusababisha majani kukauka. Upungufu mkubwa wa mazao hutokea.
Njia ya dhibiti:
kupulizia dawa ya wadudu kama AGROMETHRIN 10 EC 
kuteketeza masalia ya mazao
kutumia mzunguko wa mazao                    


Magonjwa ya vitunguu
Ugonjwa
Dalili za ugonjwa ni:-
Picha
Baka zambarau (Puple Blotch)
Ungonjwa huu una
Share on Google Plus

About CLETUSKAMANYI BLOG

0 comments:

Post a Comment